Pages

10 May 2012

Thursday, May 10, 2012

Joyous Celebration Kukanyaga Ardhi Ya Tanzania, Yatuma Mwakilishi Namna Ya Kujiunga na JC



Mmoja kati ya viongozi watatu wa kundi maarufu la muziki wa injili la Joyous Celebration pastor Jabu Hlongwane hivi karibuni aliweka wazi namna kundi hilo linavyofanya kazi kwa kugawana majukumu ikiwa ni pamoja na kutuma baadhi ya watu wao katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.Pastor Jabu aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa kupitia kipindi cha runinga ya Faith kiitwacho Praise Talk jijini London nchini Uingereza alikokuwa kwa mwaliko wa uimbaji.Amesema kundi hilo linawafanyakazi zaidi ya 80 wavitengo mbalimbali ikiwemo mavazi,muziki,matangazo na mambo mengine.Ambapo wakati huo yeye akiwa jijini London uongozi wa kundi hilo umemtuma mwakilishi wao nchini Tanzania kuangalia mazingira na mambo mengine kwakuwa kuna uwezekano mkubwa wa kundi hilo kufanya tamasha mwakani.Pastor Jabu alikuwa akijibu maswali mbalimbali aliyokuwa akiulizwa na watangazaji wa kipindi mwanadada Praise Asemota pamoja na Charles(mwanzilishi wa tuzo za gospel africa zinazofanyika London Julai) ambao kwa pamoja licha ya kutaka kujua huduma na maisha ya Pastor Jabu Hlongwane walimuuliza mambo mengi kuhusiana na kundi la Joyous Celebration.
                                                                Viongozi wa JC

ATOA SIRI ILI KUJIUNGA NA KUNDI HILO.Akijibu swali la ni sifa gani mtu awenazo ili kujiunga na kundi hilo,Pastor Jabu amesema ili kujiunga unatakiwa uwe wewe '' just be yourself'' sio kuiga kuwa kama fulani,wanatafuta mtu wa kujiunga na kundi hilo ambaye anaweza kuonyesha kitu ambacho waimbaji wa kundi hilo hawana,akaenda mbali zaidi na kutolea mfano wa pastor Agu Uche(double double) kwamba Joyous kwasasa imeamua kutafuta ladha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ndio maana wakampata Uche na sasa wanaye Mkhululi kutoka Zimbabwe kama una ndoto za kuimba kundi hilo kwa kugeza waimbaji waliopo katika kundi hilo basi sahau kujiunga nao.

                                                                    Kiongozi wa Joyous Lindelani Mkhize. 

Mfano mwingine amesema ni yeye mwenyewe uimbaji wake ni wakwake binafsi hajamuiga mtu,nao watangazaji wakamtolea mfano choirmaster bwana Lindelani kwamba uongozaji wake ni wakwake yeye mwenyewe,kisha wakamuuliza Jabu ni kwanini kiongozi mwenzake anapenda kuvaa kofia muda wote Jabu akacheka kisha akasema ile ni trade mark ya kwake kwa wataalamu wa biashara wanajua anamaanisha nini, ama kwa lugha nyepesi unaweza kusema kile ni kitambulisho chake.

Aidha amesema kwasasa wanatafuta waimbaji kutoka nchi kama Mali,Siera Leone au Cameroon kwakuwa nchi hizo zina uimbaji wao wakipekee na Joyous wamenuia kuwa kundi la Afrika.Sasa kwa Watanzania ambao wana ndoto za kutaka kuimba katika kundi la Joyous fanya mazoezi ya namna yako tumia ujuzi wako na Mungu wako sio ugeze uimbaji wa waimbaji wa kundi hilo kwani ndoto yako haitatimia hasa wakati huu ambao nafasi imeanza kupatikana kwa kundi hilo kufikiria kuja kufanya tamasha la uimbaji mwakani. 



Source: Gospel Kitaa

No comments:

Post a Comment