Pages

08 May 2012

Kutana na Lights Light Singers Kundi la Muziki wa Injili liundwalo na watoto saba wa Familia moja



Lights Light Singers ni kundi la Muziki wa Injili lenye makazi yake jijini Dar es salaam maeneo ya Kinondoni Hananasifu.Kundi hili linaundwa na ndugu wapatao saba kutoka katika wa familia moja ya Mchungaji Absolom Mwalubalile.Mchungaji Mwalubalile ni mtumishi wa Mungu anayemtumikia Mungu chini ya Kanisa la Tanzania Assemblies of GOD (TAG) Kinondoni Hananasifu.

Baadhi ya wana Lights Light Singers

 Ndugu hao ambao ni Suma ,James, Deborah,Leah, Godbless,Suzan pamoja na Jonathan, japo wameachana miaka wamekuwa kwa muda mrefu sasa hivyo uimbaji waliuanza wakiwa bado wadogo.Kwa mara ya kwanza waliamua kufanya album ya kundi hilo Mnamo mwaka 2009 ambayo waliipa jina la Fadhili za Bwana iliyokuwa na nyimbo zipatazo nane baaadhi yao ni

Uwezo
Msalaba.
Fadhili Za Bwana
Ni Utukufu Wako
YESU ANIPENDA
Usinitafute

Kwa sasa Lights Light Singers wamemaliza kurekodi album yao Mpya ya Audio ambayo wameifanyia katika studio ya Shekinah iliyoko maeneo ya Bamaga jijini Dar es salaam.Mnamo mwezi wa Tano mwishoni(May) Light Lights Singers watakuwa wakizindua album yao hiyo mpya na baada ya Uzinduzi huo watakuwa wanajiandaa kwa ajili ya kurekodi Live DVD Album.

Kundi hili limekuwa likihudumu katika maeneo mbalimbali kwa ajili  ya utukufu wa Mungu.Milango iko wazi kwa yeyote kufanya kazi pamoja na kundi hilo,unaweza wasiliana nao kupitia 0714129474 au kupitia Account yao ya Facebook ambayo ni Lights Light Singers M.

No comments:

Post a Comment