Pages

01 April 2012

Sunday, April 1, 2012

Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) Yazindulia Rasmi

Mchungaji Kiongozi Wa Kanisa la VCC ametangaza rasmi kuwa Jina la Kanisa Hilo kuanzia leo Tarehe 1 April, 2012 litakuwa likitambuliwa kama VCCT yaani Victory Christian Centre Tabernacle. Hayo aliyasema katika Uzinduzi wa Hema ya Kuabudiwa iliyozinduliwa rasmi katika maeneo ya Kawe-Mbezi Beach.


Tent hilo liliagizwa kutoka South Africa na Kufungwa na Wataalam Kutoka South Africa lina uwezo wa Kuingiza watu 1000 kwa mara moja limezinduliwa leo katika Ibada Maalum iliyofanyika katika Hema hiyo ya Kukutania.


Mbali na Rivers Of Joy ambayo ni Praise Team Ya VCCT, ibada hiyo pia ilinogeshwa na waimbaji wengine kama The Reapers, The Voice na Jennifer Mgendi.


Ibada hiyo iliyojaa Shamra Shamra kutokana na Ibada hiyo kujawa na furaha ya kuwa kwenye Hema ya Aina yake ilisababisha watu wengine kutoka machozi baada ya kuona vile Mungu alivyowavusha kutoka hatua moja kwenda nyingine.


Waumini wa VCCT wakishangilia siku ya leo kwneye Ibada hemani
Praise Team Rivers Of Joy ikiwa inajipanga kwa ajili ya Kuongoza Ibada
Mama Mchunagji Joyce Nkone ambaye ni Assistant Pastor wa VCCT akienda sawa kwenye Ibada ya leo.
Dr, Rev Huruma Nkone akienda sambamba kwenye Ibada
Ndani ya Hema siku ya leo
Dr. Rev Huruma Nkone
 Dr. Huruma Nkone akihojiwa na Waandishi wa habari
 Kitu Ndani Ya Hema
 The Reapers Choir Wakiwa hemani siku ya Leo
 Jennifer Mgendi akiwa kwenye Ibada VCCT
The Voice wakiwa sawa ndani ya Hema leo

No comments:

Post a Comment