Pages

25 April 2012

Shuhuda:Afunguliwa kutoka katika kifungo cha kula Sabuni




 Binti mmoja kutoka nchini Afrika ya Kusini, mwezi uliopita (March 2012) katika kanisa la Christ for all Nations(SCOAN),Mungu alimfungua kutoka katika kifungo cha Kula Sabuni kama chakula chake.Binti huyo alisema baada ya kufanyiwa maombi na Nabii Temitope Joshua(TB JOSHUA) hamu ya kula Sabuni haipo tena.
Kwa mujibu wa Maelezo ya Binti huyo, amekuwa akila sabuni kwa miaka 24, na alipokuwa akienda supermarket alikuwa akichukua sabuni ya mche na kula  na akasema zinaladha kama pipi.Lakini baada ya maombezi alipopewa sabuni ili aile alisema hawezi kula kwa kuwa ina harufu mbaya.Humu duniani kuna watu wenye matatizo kuliko tunavyofikiri, lakini Mungu wetu hutufungua katika hayo zaidi ya ya namna tumfikiriavyo.
Binti  huyo akiwa na sabuni kanisani SCOAN

No comments:

Post a Comment