Pages

25 April 2012

FELIS Mwambalo MUBIBYA AINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA KUANDAA NA KUSAMBAZA MUZIKI NCHINI MAREKANI.



Muimbaji mwenye vipaji mbalimbali Felis Mwambalo Mubibya ameingia mkataba na kiwanda au kampuni ya kuandaa, kutangaza na kusambaza mziki iitwayo Tate Music Group (TMG) ipatikanayo Mustang,
Oklahoma, katika Jamuhuri ya Muungano wa Kimarekani.
                                                Felis Mubibya Akiwa Ameshika Mkataba.

TMG waliamua kuingia mkataba huu na muimbaji Felis, baada ya kuupenda mziki toka kwenye a lbamu yake mpya i i twayo Jipe Moyo/Take Heart. Kazi hii ilirekodiwa na Fnouk Music Studios ya Arusha, Tanzania, East Africa na kukamilishwa au kufanyiwa mastering na Audio Recording Studio (ARS) ya Homewood, Illinois, USA. Albamu hii ambayo imekaribia steji yakuwa hewani na madukani katika kampuni hiyo inayo m’miliki muimbaji Felis TMG, na kutazamia kuzinduwa albamu hii katika tamasha kabambe itakayofanyika katikati ya mwezi Julai katika mji wa Crown Point, Indiana, Marekani. Felis anasadikika kuwa muimbaji wa kwanza wa nyimbo za Injili kutoka


Afrika mashariki na kati kuingia mkataba na TMG. Felis ni mwenyeji wa jamhuri yaki Democrasia ya Congo, mwenye nia yakufikia mataifa kupitia uimbaji wa nyimbo za Injili. Akifuata wito wa Roho Mtakatifu, aliondoka nyumbani kwao katika mji wake wakuzaliwa Bukavu, nchini Congo. Alianza safari yake huku
akihudumu katika nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Rwanda, Burundi, Uganda, na Kenya
kabla yakufanya makazi mkoani Arusha, nchini Tanzania. Jipe Moyo, ni album ya tatu (3)
yake Felis baada ya kazi yake ya kwanza iliyojulikana kama, Yuko Njiani, iliyotolewa Arusha
2006, na Yesu ni Mungu, iliyotolewa 2008.

Jipe Moyo imebeba mchanganyiko wa midundo maalum “unique blend” kutoka katika
utamaduni wa Congo na Africa Mashariki. Kwa ajili ya kufikisha Habari Njema na ujumbe
muhimu na wenye thamani, unaofariji na kuleta tumaini, pia ujumbe huu ni kwa watu wa
makabila na tamaduni zote popote duniani.

Felis alikuwa na hili lakusema :
“Jipe Moyo” ni ujumbe maalum Mungu anao sema na ulimwengu kwa sasa. Katika mambo
yote haya yanayoikumba dunia, watu wanakata tamaa, hawajui hata lakufanya au pakwenda.
Kama wewe pia unapitia hali yakukataliwa na nduguu jamaa na marafiki, au kukosa kazi na
kufukuzwa kazini, ugumu wa maisha au ugumu wakufikia malengo. Ujumbe wake Mungu
kwako leo ni huu, “Jipe Moyo!”
"Ulimwenguni mna dhiki, ila jipeni moyo; Nilishinda ulimwengu Yohana 16:3
You might also like:

No comments:

Post a Comment