Pages

10 March 2012

                            Tehila Ministry - PASTOR ISACK MALONGA


Neno la Mungu

Kila ijumaa jijini Dar es salaam maeneo ya Mbezi Tangibovu, hufanyika Usiku wa Tehila ambapo watu kutoka madhehebu tofauti tofauti hukaa pamoja na kumwabudu Mungu na kusikiliza Neno la Mungu kuanzia saa moja na nusu Usiku mpaka saa sita usiku. Ijumaa ya  jana baada ya wasaa mzuri wa kuabudu ulioongozwa na dada Annie  huku John Marco akipiga KeyBoard. Mtumishi wa Mungu Dada Jane Mutua  alifundisha kwa habari ya INTIMACY AND RULERSHIP/ LEADERSHIP akisisitiza kuwa GOD is Looking for the Worshipers.

Wakati Mtumishi wa Mungu Mathias Muhoja akimkaribisha Dada Jane Mutua alisema  huwezi kumpendeza Mungu kama hujui namna ya Kumsikiliza na kutii kile ambacho amekisema. Unaposhindwa kumsikiliza Mungu unakuwa huna Direction na kuishia kukopy vitu ambavyo wengine wanafanya kwa kuwa huna cha kwako.Unapokuwa na kitu cha kwako ambacho Mungu amesema na wewe Lazima utakuwa Mbishi, hata kama mambo hayaendi sawa lakini kwa kuwa kuna Neno la Mungu juu yako Utakaza katika kuamini kuwa Agano la Mungu aliloweka na wewe lazima lije kutimia.

Maombi yalifanyika

No comments:

Post a Comment