Pages

21 March 2012

TABASAMU LA KWELI

Tabasamu ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, maana husaidia kuficha mitazamo mingi ya watu.

¤ Tabasamu hukusaidia kunyamazisha maneno ya watu yaliyojaa uvumi na uongo.
¤ Pia Tabasamu husababisha afya nzuri mwilini mwako, mwandishi wa mithali anasema “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri bali roho iliyopondeka huikausha mifupa (Mithal 17:22).
¤ Kutabasamu mara kwa mara kunakufanya kuishi kwa muda mrefu hapa duniani.
¤ Kutabasamu kutakufanya kuepukika na msongamano wa magonjwa mbalimbali na hivyo kuifanya afya yako kuwa salama.
¤ Kutabasamu kutakufanya uwe na mafanikio mengi.. Mfano. Utafanikiwa katika kazi zako, kupendwa na watu pamoja na kufanyika Baraka kila unapokanyaga, kuwa na amani wakati mwingi,
¤ Pia kupitia Tabasamu unaweza pata Mchumba, Scholarship, kazi nzuri n.k

¤¤¤ Hivyo basi ukutanapo na msongamano wa mawazo yenye kuhatarisha maisha yako jitahidi sana kukaa katika hali ya Kutabasamu. Maana Moyo wa furaha huchangamsha uso bali huzuni ya moyo roho hupondeka..

¤ Jitahidi sana kutabasamu unapokutana na watu mbalimbali.. Maana majibu mazuri ya mtu husababishwa na Tabasamu lake.

GOD BLESS YOU.

No comments:

Post a Comment