Pages

15 March 2012

Apostle Mwingira aongelea siasa ya Tanzania


Nabii Josephat Elias Mwingira kushoto akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete


Saa nyingine najiuliza hivi nchi hii haina Serikali?, lakini nagundua kwamba nchi yeyote selikali yake ikiwa ovu, watu wake wanateseka
Ni aibu kwa wageni kuonekana wana nguvu katika nchi hii, na Raia wanaonekana kama wakimbizi katika nchi yao


Jumapili iliyopita Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa huduma ya EPHATA aliongelea kwa kifupi siasa ya Tanzania kabla hajaanza kufundisha somo lisemalo NGUVU YA MUNGU IWEZAVYO KUMSAIDIA MTU AWEZE KUTOKA MAHALI.Katika ibada hiyo iliyokuwa ikirushwa LIVE na kituo cha cha Television cha TRENET kinachomilikiwa na huduma hiyo mtumishi wa Mungu alisema

“Nchi hii sio mali ya Serikali sio mali ya chama cha siasa,ni nchi ya watanzania wenye sura ya kitanzania ambao Mungu amewaweka Tanzania. Awe mjinga,Tajiri Maskini au Mwerevu ni Kwake hapa.Inasikitisha ,ni aibu kwa wageni kuonekana wana nguvu katika nchi hii, na Raia wanaonekana kama wakimbizi katika nchi yao. Na mi nnafahamu sana wanaposikia mi naongea hivi wanatafuta kila namna kunimaliza hawawezi washindwe katika jina la Yesu”

Mtumishi Mwingira aliendelea kusema “Saa nyingine najiuliza hivi nchi hii haina Serikali?, lakini nagundua kwamba nchi yeyote selikali yake ikiwa ovu watu wake wanateseka,lakini Mungu ataiponya Tanzania. Najua kwa machozi yangu, kwa machozi yenu na machozi ya watanzania wengi ambao wanatoa machozi kwa ajili ya nchi hii, Mungu atashughulika na majambazi, wahuni wezi wala rushwa, Mungu atapunguza siku zao, katika kuishi kwao watakufa kwa kilo mbilimbili watakufa kwa presha, watakufa kwa ukimwi,kisukari yatawapunguza mpaka wafe tu,na wataondoka tu”.

Akazidi kusema “Na kwa moyo wangu wote kama Mungu alivyoniambia watawala ambao wanategemea uchawi, kuanzia wachawi na wenyewe watakufa.watanzania wenzagu mzidi kuipenda nchi yetu, mzidi kuiombea nchi yetu Mungu ataibadilisha Tanzania. Katika kufahamu kwangu sijaona chama kizuri,YESU NI MZURI.Tukimpa Yesu maisha yetu Yesu ataibadilisha Tanzania, ninaamini wakati wa Yesu kujitokeza Afrika umefika,wakati wa Yesu kubadilisha tawala za Afrika umefika.Ninaamini kwa MOYO WANGU WOTE, Human right ambazo zinazungumza u-gay hazitotokea Tanzania” alimaliza Apostle Mwingira

No comments:

Post a Comment