Pages

16 February 2012

VITA VYA KIROHO PART 1.

VITA VYA KIROHO Part 1


 Yohana 10:10 ‘Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu…
 Waefeso 6:10-18 ‘Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake, vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani 12 kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama ; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwngu wa  roho’.

 2 Wakorinto 10: 3-5 ‘Maana ingawa tunaenenda kaitka mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili,bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome); 5 tukiangusha mawazo na kila kkitu kilichoinuka kijiinuacho kinyume cha elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo.



 Siku zote jambo lolote lile linalotokea kwenye maisha ya mtu katika ulimwengu wa kimwili ujue lilianzia kwenye ulimwengu wa kiroho. Mfano ukiona wanandoa wanatengana ujue walishatengana kwanza katika ulimwengu wa roho ndipo sasa inadhihirika kwenye ulimwengu wa kimwili.  Kwa hiyo siku zote vita kati ya Mkristo na Shetani inapigwa katika ulimwengu wa roho kwanza.   

 Mtu akimshinda shetani na mapepo yake kwenye ulimwengu wa roho ujue hata kwenye ulimwengu wa mwili atashinda. Naam ni katika ulimwengu wa roho ndipo Mungu anapotaka watoto wake tuliokoka tujue namna ya kuvipiga vita dhidi ya shetani. Naam tukishindwa kwenye ulimwengu wa roho na kwenye ulimwengu wa kimwili tutashindwa na tukishinda kwenye ulimwengu wa  roho na kwenye ule wa mwili tutashinda.

 Ukweli huu tunaupata kutoka kwenye andiko la 2Wakorinto 10:3-5, maana Biblia inasema silaha zetu si za mwili, ina maana ni za kiroho, sasa huwezi kutumia silaha za kiroho kupigana vita ya kimwili

No comments:

Post a Comment