Pages

23 February 2012

MGENDI NDANI YA GEMU LA GOSPEL

Salamu za Jenifer Mgendi kwa Wapenzi wa Muziki wa Injili na Filamu za kikristo



Jenifer Mgendi

Salaam nyingi ziwafikie wapendwa, naamini kwa neema ya Mungu mmeuona mwaka. Mimi pia, namshukuru Mungu.

Nachukua fursa hii kuwajulisha nilipo na ninapokwenda kwa mwaka huu na naomba  kama kawa muwafikishie watanzania na wasomaji wenu kwa ujumla mambo haya. Natanguliza shukurani zangu za dhati.

DHAHABU, Hii ni albamu yenye mkusanyiko wa baadhi ya nyimbo zangu za zamani kama vile Nini?, Nimrudishie nini Bwana, Nitafika lini?, Mbona washangaa njiani. Ulinipa sauti na nyinginezo ambazo zilitamba miaka ya 2001 na kurudi nyuma hadi mwaka 1995. Albamu hii tayari ipo madukani katika mfumo wa audio cd yaani ni ya kusikiliza. Maandalizi ya video hii yanafanyika na panapo manajliwa mwezi Agosti itakuwa imekamilika.

TEKE LA MAMA
, Filamu hii ipo madukani na imewashirikisha watu mbalimbali kama Bahati Bukuku, Christina Matai, Senga, Lucy Komba na Godliver a.k.a Bibi Esta. Sio filamu ya kukosa kuangalia na uzuri wake unaweza kuiangalia ukiwa umetulia na familia yako bila kuwa na wasiwasi wa kuanza kuwatuma watoto dukani ili wasione picha chafu.

SHEREHE ZA MIAKA 15 YA HUDUMA
Panapo majaliwa na Mungu, natarajia kufanya tamasha la kusherehekea na kumshukuru Mungu kwa miaka 15 tangu nianze huduma ya uimbaji. Tamasha au sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 05 Agosti, 2012 katika ukumbi wa Landmark Hotel.Video ya album ya Dhahabu itazinduuliwa siku hiyo pia.
 Maandalizi ya tamasha hili yanaendelea na litapambwa na waimbaji mbalimbali watakaoimba live siku hiyo. Sio siku ya kukosa na wote wenye mapenzi mema wanaombwa kujitokeza kwa wingi. Tutaendelea kuhabarishana kuhusu tukio hili kadiri siku zinavyoendelea.

ALBAM MPYA, Maandalizi ya album mpya yanaendelea moyoni lakini rasmi kabisa yataanza mara baada ya tamasha la mwezi wa Agosti na album hii mpya inatarajiwa kuingia sokoni mwezi Aprili mwaka 2013, tukijaliwa uzima.

Ni hayo tu ndugu zangu nawatakia siku njema

No comments:

Post a Comment