Kuna watu wanampenda Bob Marley ama wanasema wanafuata nyayo au kuiga mfano wake, lakini ziko habari kwamba Bob Marley kabla hajafa alimpokea Bwana Yesu na kubatizwa kuwa muumini wa Orthodox na siyo Haile Selassie.
Alipokuwa katika mahojiano Askofu aliyembatiza Marley, Abuna Yesehaq wa kanisa la Ethiopia Orthodox, alisema Marley alikuwa mtoto wa Mungu tofauti na watu walivyomuona.
Aliendelea kusema “Ugonjwa wake wa kansa ulikuwa sababu kubwa ya yeye yeye kumpokea Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Watu wengi walidhani alibatizwa kwa sababu alijua angekufa, lakini haikuwa hivyo, alibatizwa kwasababu hakuwa na msukumo kutoka kwa yeyote na alipobatizwa aliikumbatia familia yake na kulia kwa nusu saa.”
Marley alibatizwa tarehe 4 Novemba 1980 na alifariki 21 May 1981 akiwa na miaka 36.
Tukiachana na habari ya Robert Nesta Marley au Bob Marley, Kuna dini ya marastafari na washirika wake tunao mitaani ambapo kwa asilimia kubwa ni vijana, Je dini hii ya marasta wanaamini nini? na rasta zinahusiana vipi na kuvuta Bangi?
No comments:
Post a Comment