Pages

20 January 2012

Sonnie Badu atoa Ushuhuda namna mtu alivyoponywa Kansa na Mwingine Utasa wakati akimuabudu Mungu


Sonnie Badu Ni Mwanamuziki wa Injili kutoka nchini Ghana Barani Afrika. Katika moja ya Ziara zake za kitumishi alitoa ushuhuda huu na kusema.

 “Jumapili  moja wakati  nikiuimba wimbo wa “Covenant Keeping God”  kanisani, ndani ya ibada hiyo  kulikuwa na Mwanamke aliyekuwa akitegemea kwenda kufanyiwa operation jumatatu (Kesho yake), mama huyo alikuwa akisumbuliwa na kansa ya titi. Mungu alisema na Mimi kuwa Muangalie huyo mwanamke na mpe Leso yako(kijitaulo cha kufutia uso-Face Towel).

Nilichokifanya nilimpa taulo ile naye akaiweka mahali palipokuwa na kansa. Wakati naendelea kuimba sikujua kuwa kuna uponyaji ulikuwa ukiendelea katika Mwili wa Mwanamke yule. Siku ya pili yake ndiyo ilikuwa appointment yake ya kufanyiwa operation.  Alipofika madaktari walipompima walimuuliza  nini kimetokea? hauna kansa tena, mpaka leo mwanamke Yule ni Mzima na hana kansa tena.

Mwanamke mwingine yeye alikuwa hajapata mtoto kwa Miaka Saba, wakati nauimba Wimbo huu Mungu alimponya Ugumba ,akaweza kushika Mimba na akapata mtoto, Our GOD is Covenant Keeping GOD”. Sonnie alisema Mungu wetu ni Mungu Mwenye kushika Maagano.

Sonnie Badu kwa Muda mrefu sasa amekuwa akimtumikia Mungu Barani ulaya. Tofauti na uimbaji Sonnie humtumikia Mungu kama mchungaji  na Kiongozi wa Huduma yake ya Sonnie Badu Ministries.Kwa sasa Sonnie ndiye Mwanamuziki bora wa Injili Barani Afrika  2010/2011 nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Ucheagu (Uche wa Double-Double) kwa miaka miwili mfululizo .


No comments:

Post a Comment