Pages

29 January 2012

Mwimbaji wa nyimbo za injili Christina Shusho

Kwa muda mrefu sasa media nyingi za Tanzania zimekuwa zikiplay nyimbo za kundi la Christ Ambassadors Choir. Album ya kundi hilo kutoka Kigali Rwanda  iliyopewa jina la KWETU PAZURI (Video na Audio) kwa takribani miezi mitano  toka August 2011 imekuwa ikisikika sio tu kwenye media bali hata majumbani, mitaani na sehemu mbalimbali. Kitendo cha Christina shusho kuingiza sokoni album yake ya VIDEO iitwayo NIPE MACHO mnamo tarehe  tarehe 23/dec/2011 imeonekana kuteka hisia za wengi kwa utukufu wa Mungu.
Katika Video Album hiyo ya Shusho iliyofanywa tena na kampuni ya MBC HOTMEDIA, nyimbo ya kuabudu iitwayo NATAKA USHIRIKA NA WEWE ndiyo inayoongoza kuchezwa katika media mbalimbali ambapo tar 1jan 2011 nyimbo hiyo pamoja na Nyingine iitwayo NINA WIMBO zilichezwa kwa mara ya kwanza na katika kituo acha Television ya CITIZEN cha nchini Kenya katika kipindi cha RAUKA Kinachotayariswha na K-KREW.
Wakati Christina Shushu ameuanza Mwaka huu wa 2012 kwa kishindo kwa album yake hiyo ya Video, nguli mwingine wa Muziki wa injili nchini ROSE MUHANDO na yeye Mwaka huu wa 2012 anatarajia kuingiza sokoni album yake ya Video iitwayo” UTAMU WA YESU” baada ya ile ya Audio aliyoitoa mapema mwaka jana. Kufanya Vizuri kwa Video album hii ya NIPE MACHO ni hatua ya kwanza kabla hajaachia Video album yake nyingine iitwayo KWA KANISA LA KRISTO.




Viongozi wa Dini Nchini Uganda walalamikia Kitendo cha Mchungaji Kumwagiwa Tindikali
Viongozi wa Dini nchini Uganda wamelalamikia kitendo kilichofanywa na watu wasiojulikana cha Kumwagia Tindikali(Acid) usoni Mchungaji Umar Mulinde wa kanisa la GOSPEL LIFE CHURCH lililoko jijini kampala nchini humo.Kitendo hicho kilifanyika siku ya mkesha wa Christmas (Christmas Eve)  mara baada ya kumaliza kuongoza Ibada kanisani hapo.
Mch Umulinde alipata shambulio hilo majira ya saa tisa alfajiri baada ya mkesha kumalizika na baadaye aliwahishwa kupelekwa Hospitali na washirika wake katika International Hospital Kampala. Kwa Mujibu wa New Vision  Babaake na Pastor Umar alikuwa ni Imam na Mch Umar Mwenyewe alikuwa Sheikh kabla hajamkabidhi Yesu Maisha kama Bwana na Mwokozi wa Maisha Yake.

Baada ya Mch Umar kuokoka alipata vipingamizi vingi kutoka katika familia yake yenye msimamo mkali na dini ya Kiislamu. Shambulio hilo limepelekea Mchungaji Umar  kupoteza uwezo wa kuona wa jicho lake la kulia, huku upande wa kulia wa sura yake ukiwa umedhurika.

Akielezea tukio hilo akiwa hospitalini Mch Umar anasema baada ya kutoka kanisani kuna mtu mmoja alinifata akijifanya mkristo na kuniita kwa nguvu Pastor,  Pastor, Pastor, nilipogeuka kuangalia ninani anayeniita  ndipo aliponimwagia Tindikali usoni, nilipogeuka baada ya kumwagiwa mtu mwingine akanimwagia tena tindikali mgongoni kisha akakimbia akisema “Allah Akbar”( Mungu Mkubwa)”

Mch Umar amekuwa akiendesha mikutano ya Injili na kuwaambia watu wote hususani waislam wamgeukie kristo kama alivtofanya yeye. Kwa muda wote ambao yuko Hospitali Mch Amar amekuwa akiuguzwa na mkewe ambapo watumishi wengi nchini humo wamefika na kumuangalia pamoja na kufanya maombi.

Mchungaji Umar Mulinde kabla hajashambuliwa kwa Tindikali



Mchungaji Umar Mulinde akiwa katika moja ya mikutano yake akitangaza Habari njema za Ufalme wa Mungu

No comments:

Post a Comment