Pages

19 February 2014

Step Up.....Hilda Nchunga Mwanamuziki anayewaza Kufika Mbali





Ze Blogger: Wasomaji watatami kusikia majina yako Kamili

Hilda: Majina yangu kamili ni Hilda Nchunga

Ze Blogger: Ulizaliwa wapi na ni Mtoto wa ngapi Kuzakuwa kwenye familia yenu?

Hilder: Nilizaliwa katika Mkoa Wa kigoma na kwa sasa niko Mkoani Morogoro kwa ajili ya masomo. Mimi ni mtoto wa 3 kuzaliwa kati ya watoto wanne wa mzee Isaack Nchunga.

Ze Blogger: Kwenye kizazi chetu cha sasa Vijana wengi sana hawapendi kujishughulisha Kihuduma wanapenda tu kuingia na kuondoka wewe Kanisani unajishughulisha na nini?

Hilda:Nikiwa kanisani nafanya kuduma ya praise team ktk kanisa la TAG Bethel Rivavil Temple mjin morogoro, Mungu ameweka kwangu huduma ya Kusifu na Kuabudua na Kipaji cha Kuimba.

Ze Blogger: Maelezo yako ya awali ulieleza kuwa uko morogoro Kimasomo unasoma wapi?

Hilda: Mimi ni mwanafunzi katika chuo cha St.Augustine branch ya Morogoro.

Ze Blogger: Maisha ni mapambano na achievements and falls je umewahi fanya kitu ukajisikia hapa sasa nimefanikiwa?

Hilda: kitu nimewahi fanya kwenye maisha ni kukamilisha albam yangu ya 1 ya Hosana sababu kwa was expensive but with God help nilifanya, kitu naweza sema katika albam hii ya Hossana, ni albam yenye nyimbo 8 zilizojaa Neno la Mungu ndani yake.

Ze Blogger: Kati ya Changamoto kubwa za Wanamuziki wa Tanzania ni namna ya kusambaza kazi zao je wewe nani anakusambazia zako? na je ni audia ama ni DVD?

Hilda:Albam hiyo ipo katika mfumo wa audio na inapatikana kupitia mimi mwenyewe ninapoenda fanya huduma sehemu mbalimbali, kuhusu kufanya video ninajiandaa kwa kuifanya baada ya kumaliza masomo mwez wa 6.

Mungu akubariki Hilda.

Asante Ubarikiwe.

GLORIOUS YAANZA USIKU WA MATUMAINI KWA KISHINDO

Usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa 92 Hotel ama Shalom Tabernacle church kulifanyika mkesha wa kwanza wa aina yake ufahamikao kama Motivational Friday Night chini ya kundi matata la injili nchini la Glorious Worship Team, ambao wamerejea tena kuwakusanya wapendwa na marafiki zao kila Ijumaa kuanzia jana na ijumaa zote zinazokuja kwahiyo mdau usikose kila siku za ijumaa ndani ya Hotel 92 karibu na Sansiro Shekilango jijini Dar es salaam.
Tazama picha japo kwa uchahe, GK itakupasha kilichojiri kwa upana ikiwemo video za tukio hilo


Barikyiz na Paul Clement


Blogger Rulea Sanga akizungumza jambo pembeni Paul Clement akimsikiliza


Hakika ilipendeza

MD wa GWT Immanuel Mabisa akiliungurumisha bass

GWT wadada wakienda kizimbabwe zaidi.



Ndani ya uwepo wake ni rahaa