Pages

05 August 2012

Launching Ya Let It Rain Ya Sara Shilla Next Level


Siku Ya Leo Katika Ukumbi wa Banora Maeneo Ya Survey Karibu na eneo la Mlimani City Mwanamuziki Wa Injili Sarah Shilla amezindua Albam Yake ya Kwanza yenye jina la “Let It Rain”.
 Mwenge Praise Team wakihudumu Siku Ya Leo
 Rivers Of Life Kutoka DPC chini Ya Pastor Safari Wakihudumu Siku Ya leo
Eunice akiwa na Kundi Lake
Katika Uzinduzi Huo Uliopambwa na vikundi mbalimbali vya uimbaji ulifana kwa aina yake katika Ukumbi huo wa Kisasa kabisa Jioni ya leo. Kati Ya Vikundi vilivyo hudumu siku ya leo ni Mwenge TAG Praise Team ambao waliongoza Kusifu na Kuabudu, wengine ni Rivers Of Life Wa DPC, Rivers Of Joy Wa VCC, Eunice and Miriam Lukindo Wa Mauki na wengine wengi
 Miriam Lukindo wa Mauki ndani ya Banora
Rivers Of Joy Kutoka VCC wakiwa Ndani ya Kumsindikiza Sarah Shilla Kwenye Launching ya albam. 

Mshehereshaji Mashuhuri jijini Dar, Mc King Chavalla ndiye aliyekuwa akiongoza shughuli nzima ya Jioni ya leo. Mbali na Kuongoza event hiyo pia Mc huyo alifanya Comedy kama ilivyo kawaida ya Mc huyo the King Of Stand Up Comedy.
 Mc wa Event King Chavala akiwa Kikazi Zaidi Siku Ya Leo
Pastor Safari Akifungua event ya Siku Ya leo.
Mwanamuziki wa Injili alipanda Jukwaani Majira ya Saa 12 jioni kwa style ya aina yake na kuhudumu nyimbo 5 mfululizo Jukwaani. Kisha Rev Dr. Huruma Nkone Alibariki Albam hiyo ya "Let It Rain In His Presence".
Rev. Dr. Huruma Nkone akiwa ndani ya Banora Siku Ya leo.

Blog Inatoa Big Up Kwa Sara Shila Kwa Siku ya leo Kufikia hatua hiyo.
 Watu Peopleeeeee Hand Uuuuuuuuuuup
 Papaa Ze Blogger Kama Kawa Akiwakilisha Siku Ya leo
 Without Caption Jana Na Leo....../....
 Sara Shilla Akihudumu Siku Ya Leo
 Tehe tehe Hawa Ndo Walibeba CD, Sijui Waliimba Baadae???
 Rev. Dr. Huruma Nkone akizindua Albam hiyo Siku Ya Leo Kwenye Ukumbi Wa Banora.

02 August 2012

Love Tanzania Festival kuyakutanisha zaidi ya Makanisa 800 nchini



Miwani 10,000 za kusomea kugawiwa Bure
Wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa serikari kuinjilishwa kupitia Evening Dinner
Kikundi maalumu cha Michezo ya Baiskeli kuonyesha ufundi wa kuchezea baiskeli
Tofauti na Donnie Moen, Nicole C Mullen  ,Christina  Shusho,John Lissu,Pastor Safari Paul wa DPC kuongoza Love Tanzania Festival Praise Team

Love Tanzania Festival ni kusanyiko kubwa la kihistoria litakalofanyika kuanzia tarehe 11-12/08/2012 katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa saba mchana mpaka saa 2 Usiku.Kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa kusanyiko hilo Brother Prosper Mwakitalima ameiambia Hosanna Inc kuwa katika kufanikisha kusanyiko hilo makanisa zaidi ya 800 yameshiriki katika maandalizi ya tukio hilo maalumu lenye lengo la kuwakutanisha watu wa dini,kabila,rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu.

Kwa mujibu wa Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa jamii ya Tanzania.

Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.

Tarehe 5 August  7:00Asbh – 10.00 Asbh
Mbeba maono wa Love Tanzania Featival  mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada zote mbili katika kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)

Muimbaji mashuhuri Nicole C Mullen atahudumu

Tarehe 7 August 10Asbh
Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Confference) katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE  kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.

Tarehe 8 August  12:00 jioni
Katika Ukumbi wa Karimjee Hall kutafanyika hafla ya chakula cha jioni ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na injili ya Yesu kristo.

Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni
Kutafanyika maozoezi(Rehesal)ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX  kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe 11-12.



VITUO MAALUMU KWA AJILI YA CLINIC YA MACHO
Love Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia neno la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni kama ifuatavyo.

Kituo 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA
Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)
Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti
Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni

Kliniki zote hizi zitakuwa zinaanza saa nne asubuhi mpaka saa kumi jioni

Donnie Moen kuhudumu