Pages

02 July 2012

Filamu Ya Kikristo Kuzinduliwa Ndani ya FoF Anniversary Makumbusho Kijitonyama

Kamati Ya FoF Moja Juu Wakionesha Ishara ya "Moja Juu" Itakavyokuwa ikitumika ndani ya Event.

Ilianza kama juzi juzi lakini Friends On Friday wiki leo inatimiza Mwaka mmoja kamili, Mwaka jana tarehe 2 July, 2012 FoF ilichukua Mkondo wake katika jiji la Dar-es-Salaam kama idea mpya kabisa katika ulimwengu wa Kikristo, mpaka sasa tunasema ni Ebeneza, Sizon Moja Juu Kwa Mungu, ndio Maana theme ya Safari hii ni "FoF Moja Juu". Kwa Yeye Muweza wa yote.
                       Business Analyst and Creativity Prosper Mwakitalima akionesha FoF Moja Juu

Katika Kunogesha FoF Anniversary FoF Arusha, FoF Zanzibar, FoF Mbeya Watakuwa ndani ya Jiji la Dar-es-Salaam kwa ajili kusheherekea FoF Dar kutimiza Mwaka Mmoja.

Mbali na hiyo Msemaji wa Kamati ya Maandalizi Ya FoF Mc. Antony Luvanda amesema "This Time FoF imekuja na ubunifu wa hali ya Juu, kwanza tumebadilisha Venue ili tuwe na Venue kubwa zaidi lakini pia kuondoa Mazoea, Pili FoF Imebadilisha aina ya Vyakula, this time katika FoF tutakuwa na Starter ya Chakula ambapo Vegetable Soup Pamoja na Mtori vitatolewa kwa Watu wote, ila Menu pia imeboreshwa kwa kiwango cha juu sana, Mbali na Shughuli nzima kuwa chini ya Mc Pilipili na Papaa Ze Blogger lakini kwenye Comedy tumeleta machine mpya inaitwa "Mlugaluga", Upande wa Burudani Wapenzi wa Sebene this time tuko na Regraaaant Pastor Wambura, Kwenye Kwaito, tutakuwa na Miriam Lukindo wa Mauki, Kwenye Slow Music tutakuwa na Sarah Shilla, kwenye Hip Pop tutakuwa na Elandre pamoja na Amani Kapama, Talks pale kati atafanya Chris Mauki"
                                                  Papaa Ze Blogger akionesha FoF Moja Juu

Blog ilipotaka kujua kutoka kwa Msemaji huyo wa FoF kama kuna kitu chochote Kipya, Mc Luvanda alisema "FoF ubunifu ndio jadi yetu, Safari hii tunatupia kwanza Mtupio mwekundu (color of the event), tumekuwa na majina mengi sana ya ubunifu kama vile, FoF Kitu Kati, FoF Vibration, FoF Whitepart, this time tunasema FoF Moja Juu, Kwa mara ya kwanza tutakuwa na FoF Fashion Show ambapo wadau mbali mbali wa FoF wataonesha Mitupio yote tuliyowahi kuvaa kwenye FoF Zilizopita, mbali na hapo tutakuwa na     FoF Surprise, Kwa Mara ya kwanza Tutazindua Filamu Ya KiKristo ndani ya FoF, na pia tutakuwa na Anniversary ya Blog ya Uncle Jimmy, Fof Ya Safari hii itakuwa tight sana kupita maelezo ni burudani kufurahi mwanzo mwisho"
                                                                  FoF Moja Juuuuu, Uncle Jimmy

Mc Luvanda alimaliza kwa kusema "Safari hii FoF Anniversary ni raha Kamili, FoF Moja juu".

                                                      We are One, FoF Moja Juu
 Kushoto ni Prosper Mwakitalima, Mc Luvanda, Clara kolle, Chris Mauki, Renee Lyatuu, Godwin Protace na Uncle Jimmy
                                         Prosper sijui alikuwa anasema nini hapa sikumbuki
                                                                   FoF Moko
                                            FoF Moja juu